下载 APKPure App
可在安卓获取Tafakari Injili的历史版本
Kuza na kuimarisha imani yako kwa kusoma neno,kujibu maswali ya biblia na Nyimbo
Hii ni app ambayo imeandaliwa mahususi kwa lengo la kusaidia mkristo kukua kiroho kupitia vipengele mbalimbali vilivyo jumuishwa ndani yake ikiwa ni pamoja na Kipengele cha :
1:Tafakari Fupi
Kutoka katika sura fulani ya biblia na kulingana na ROHO MTAKATIFU atakavyotuongoza tunapata tafakari ya neno la Mungu ambayo inatupa uelewa wa kina kuhusu jambo fulani katika maisha, kwa leno la kukuza imani na kutupa muongozo wa nini tufanye ili katika maisha yetu tuweze kuenenda sawa na mapenzi ya Mungu.
2:Masomo
Tunatazamia kuwa na masomo yanayo husu maeneo mbalimbali katika Imani na maisha, ambayo yatakuwa na mtiririko mzuri kuanzia sehemu ya kwanza Hadi ya mwisho. Kwa mfano tunaweza kuwa na masomo yanayohusu "IMANI" , "NGUVU YA DAMU YA YESU" ,"MALANGO" , "NDOA","MALEZI NA FAMILIA "Hivyo kipengele hiki kitatoa fursa za kuelezea kwa kina somo hatakama linavipengele 7 au zaidi vyote vitachambuliwa katika mtiririko mzuri.
3:Aya ya siku/ujumbe wa siku
Kupitia app kila siku utakuwa unapokea Aya kutatoka sura tofauti tofauti za biblia Kwa lengo kutiana moyo, kukumbusha ahadi a Mungu,kukumbusha maangizo ya Mungu na kwa ujumla wake kukuza Imani kama mtoto wa Mungu.
Unaweza kutumia aya hizi kumshirikisha ndugu, rafiki ,jamaa na watu wengine, kuwainjilisha,kuwaongoza na kuwashauri ikiwa wapo kwenye uhitaji wa namna hiyo, tukizingatia kuwa uhitaji wetu kiroho na kimwili ni tofauti kwa kila mtu na sio watu wote wana maandiko ya kutosha ndani yako ambayo yanaweza kuwasaidia kuvuka katika changamoto mbalimbali ama kuzitumia kumshinda shetani.
4:Game/mchezo
Huu ni mchezo wa maswali na majibu kutoka katika sura mbalimbali za biblia , ambazo zimegawanyika katika makundi matatu,
-- Moja maswali kutoka agano jipya,
-- Pili maswali kutoka Agano la kale na
-- Tatu mchanganyiko wa Maswali kutoka Agano jipya na la Kale.
Lengo kubwa ni kuongeza uelewa na ufahamu katika kusoma biblia Kwa watoto na watu Wazima pia ambao watakuwa na swali fulani ambalo wanaweza kujibu na kupima uelewa wao katika maandiko.
5:Nyimbo
--Tunatazamia kuwa na Nyimbo nyingi na zakutosha ambapo watu wanaweza kusikiliza na kupakua bila shida yoyote.
6:Kipengele Cha mawasiliano
Hapa tutajikita zaidi katika masuala ya Maoni,ushauri na maswali ikiwa mtu anahitaji kufanya hivyo, Basi uwanja huu utamfaa sana.
Zab 54:4
Tazama, Mungu ndiye anayenisaidia; Bwana ndiye anayenitegemeza nafsi yangu.
Flp 4:13
Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
Tuombeane katika kuitenda kazi ya Bwana.
Mungu asema: “Nitakufunza na kukuonesha njia unayopaswa kufuata. Nitakushauri kwa uangalifu mkubwa.
Last updated on 2021年11月26日
Bugs fixed, and functions improved
Tafakari Injili
1.0 by AlberaInfoTech
2021年11月26日